Mwakilishiwadi wa wadi ya Kogrogocho katika kaunti ya Nairobi Absalom Odhiambo ameshtakiwa kwa kosa la kutoa matamshi ya uchochezi katika mkutano wa kisiasa ulioandaliwa na muungano wa Azimio la umoja tarehe 25 mwezi jana.

Odhiambo ambaye aliwasilishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Milimani Lukas Onyina, alikuwa ameachiliwa huru mwishoni mwa wiki jana baada ya majaji waliokuwa katika kesi hii kusema kuwa hakukuwa na sheria yoyote ambayo ingeruhusu kushtakiwa kwa mwanasiasa huyo wa mrengo wa upinzani.

Odhiambo hata hivyo alikamatwa tena na kufikikishwa mahakamani hii leo na kusomewa mashtaka 2 ya kukusudia kuchochea wanajamii, mashtaka ambayo aliyapinga na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja.

Wakili wa mshtakiwa Danstan Omari alikaribisha uamuzi huo akisema kuwa serikali inapanga njama ya kuwadhulumu wanasiasa wanaoshirikiana na upinzani.

February 6, 2023