Boniface kARIUKI

    Mchuuzi Boniface Kariuki, ambaye alipigwa risasi na afisa wa polisi majuma mawili yaliyopita, ameaga dunia.

    Akithibitisha kifo hicho hapo jana, babake marehemu, Bw. Jonah Kariuki Nyambura, alisema mwanawe alifariki mwendo wa saa tisa na robo alasiri, saa chache baada ya madaktari kutoa taarifa kwamba ubongo wake ulikuwa umekufa.

    Boniface alipigwa risasi kwa karibu na afisa wa polisi wakati wa maandamano ya kupinga kile waandamanaji walikitaja kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi na maafisa wa usalama. Maandamano hayo yaliandaliwa baada ya Mwanablogu Albert Ojwang kuuwawa na maafisa wa polisi baada ya kukamatwa.

    SOMA PIA: KNH yatoa taarifa kuhusu hali ya mfanyabiashara aliyepigwa risasi.

    Kariuki alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) cha KNH, ambako alifanyiwa upasuaji mara mbili katika jitihada za kuondoa vipande vya risasi kwenye ubongo wake.

    Bw. Kariuki ametoa wito kwa vyombo husika kuhakikisha haki inatendeka kwa kuwachukulia hatua za kisheria maafisa waliohusika na tukio hilo.

    July 1, 2025

    Leave a Comment