BY ISAYA BURUGU,31ST OCT,2023-Mahakama kuu ya Shanzu kaunti ya Kilifi imemwachilia huru mhubiri Ezekiel Odero na faili ya kesi yake kufungwa rasmi.

Hii ni baada ya upande wa mashataka kusema kuwa uchunguzi dhidi yake ulikuwa umekamilika na faili ya kesi dhidi yake kufungwa.

Hakimu mkuu Joe Omido amesema kuwa amemwachilia mhubiri huyo katika kesi iliyowasilishwa na maafisa wa polisi kutaka achunguzwe kuhusiana na mafundisho ya itikadi kali.

Odero alikuwa akihusishwa na mhubiri bandai Paul Mackenzie wa good news international ambaye anatuhumiwa kusababisha vifo vya Zaidi ya watu mia tano kule shakahola kupitia mafundisho yake ya kupotosha.Oderoa amekuwa akichunguzwa tangu mwezi Mei mwaka huu.

 

 

 

 

 

 

October 31, 2023