BY ISAYA BURUGU 12TH JAN 2022-Sasa taarifa zimeibuka  kwamba Mwanaume aliyefungwa maisha hapo jana na mahakama ya Narok baada ya kukiri kumuoa na kumpachika mimba msichana mwenye umri wa miaka 9 ni raia wa taifa jirani la Tanzania.

Mmoja wa viongozi eneo hilo la entasekera na ambaye kwa wakati mmoja alikuwa diwani mzee Joseph ole Kuaet anadai kwamba mzee huyo ni wa kutoka kijiji cha Naan eneo la loliondo kwenye taifa la Tanzania.mzee kuaet ameongeza kuwa  kwamba ni familia anayoielewa barabara  kwani ni majirani wake anakoishi pia katika mpaka wa kenya na Tanzania .

Anadai kuwa  mzee huyo aliogopa kujitambulisha kama raia wa Tanzania alipompeleka mtoto huyo asaidiwe kujifungua katika hospitali ya rufaa ya narok.Aidha  kiongozi huyo amedai pia kwamba mzee huyo ana matatizo ya kiakili.

 

 

January 12, 2023