Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo amepoteza maisha yake kwa njia isiyo ya kawaida katika tukio la kuhuzunisha kwenye kituo kimoja cha mafuta mjini Narok. Tukio hilo limetokea baada ya gurudumu la gari alilokuwa akilijaza pumzi kulipuka ghafla, na kumwangusha na kumsababisha kufariki papo hapo.

Kamanda wa Polisi katika eneo la Narok ya Kati, John Momanyi, amethibitisha tukio hilo la kuhuzunisha. Kulingana na kamanda huyo, mwanaume huyo alikuwa akiendelea na shughuli ya ukarabati wa gurudumu hilo, na baada ya kukamilisha ukarabati, alianza kujaza pumzi gurudumu hilo. Katika harakati hizo, gurudumu hilo lililipuka ghafla likamrusha juu kisha akaanguka kwa kichwa nakuaga dunia mara moja.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika makafani ya Hospitali ya rufaa ya Narok. Kamanda wa polisi ametoa wito kwa watu wanaofanya kazi kama hiyo kuwa waangalifu na kuweka kipaumbelesuala la usalama wao wakati wanapotekeleza majukumu yao. Amewashauri kutumia vifaa vya kazi salama na kufuata taratibu za usalama zinazohusiana na kazi hiyo.

 

Share the love
October 31, 2023