odpp ocs-talaam

    Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) imeidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi ya maafisa watatu wa polisi pamoja na watu wengine watatu, kufuatia kifo cha mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang.

    Katika taarifa iliyotolewa na ODPP hapo jana, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Mamlaka Huru ya kutathmini utendakazi wa Polisi, IPOA.

    Maafisa wanaokabiliwa na mashtaka ni pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Central, OCS Samson Kiprotich Talaam, ambaye kwa sasa anazuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Nairobi; Konstebo James Mukhwana, ambaye alitoa ushahidi kwa IPOA akieleza jinsi alivyoagizwa kupanga kupigwa kwa marehemu Ojwang’; na Peter Kimani.

    SOMA PIA: IPOA yathibitisha kujitolea kwake kushughulikia kesi za polisi.

    Wengine waliotajwa ni John Ngigi Gitau, Brian Mwaniki Njue, na Gina Ammitou Abwao.

    Mamlaka huru ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA ambayo imekua ikichunguza mauaji haya, imeeleza kwamba imepata Ushahidi dhabiti ambao imewasilisha kwa ofisi ya ODPP.

    June 24, 2025

    Leave a Comment