BY ISAYA BURUGU 24TH AUG 2023-Padri Micheal Muriuki aliyetekwa nyara jana nyumbani kwa wazazi wake eneo la Mau Narok amepatikana akiwa salama.Padri huyo anaripotiwa kupatikana huko Kaptembwa Nakuru magharibi hivi leo asubuhi akiwa amefungwa  kwa Kamba.Amekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Nakuru.

Padri huyo anasemekana kutekwa nyara  nyumbani kwa wazazi wake mwendo was aa mbili za usiku wa jana na watu wasiojulikana  waliotumia gari aina ya Subaru forester likiwa na nambari za usajili KDK 353L na Kwenda naye kutumia  Barabara ya Elementaiata.

Ripoti za polisi zinaonyesha ishara za simu yake ziligunduliwa  katika maeneo kadhaa ndani ya mji wa Nakuru na gari lake lilipatikana mjini Nakuru saa 9:30 za usiku  wa kuamkia leo, likiwa limetelekezwa katika barabara ya Ogiligei.

Aidha  zaidi ya Ksh.100,000 zilitolewa kutoka kwa akaunti zake kadhaa katika maeneo tofauti mjini na kulingana na polisi, gari hilo lilipatikana likiwa limetelekezwa huku  injini yake kuachwa ikinguruma.Kasisi huyo alihamishwa hivi majuzi hadi parokia ya Holy Cross Nakuru kutoka Elburgon huko Molo.

 

.

Share the love
August 24, 2023