Fr. Vincent Odundo

    Baba Mtakatifu Papa Leo XIV amemteua Padre Vincent Ouma Odundo kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Kisumu.

    Kabla ya uteuzi wake, Padre Odundo alikuwa akihudumu kama Vika Jenerali wa Jimbo Kuu Katoliki la Kisumu, sambamba na majukumu yake ya kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mtume, Magadi.

    Padre Vincent Ouma Odundo alizaliwa mwaka wa 1978 jijini Kisumu. Alipata mafunzo ya falsafa katika Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mabanga, kabla ya kuendelea na masomo ya theolojia katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas jijini Nairobi.

    Alipokea daraja takatifu ya upadre tarehe 20 Februari 2008 katika Jimbo Kuu Katoliki la Kisumu.

    Uteuzi wa Padre Odundo kama Askofu Msaidizi ulithibitishwa rasmi na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Kisumu, Mheshimiwa Maurice Makumba, ambaye aliwatangazia waumini habari hiyo, akitaja huduma na uongozi wake wa kichungaji kama mchango mkubwa kwa Kanisa.

    December 15, 2025

    Leave a Comment