Papa leo

    Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika maeneo yote yenye migogoro duniani wakati wa sikukuu ya Krismasi.

    Akizungumza kutoka kwenye makazi yake ya mapumziko nje kidogo ya mji wa Roma, Papa Leo amesema anarejelea tena ombi lake kwa watu wote wenye nia njema kuhakikisha Krismasi inakuwa siku ya amani. Amesema hata kusitishwa kwa mapigano kwa muda mfupi ni ishara ya heshima kwa siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

    Baba Mtakatifu ameeleza masikitiko yake makubwa kuhusu kuendelea kwa vita nchini Ukraine, akisema ni jambo la kusikitisha kwamba Urusi imekataa kusitisha mapigano hata wakati huu wa Krismasi.

    Papa Leo amesisitiza kuwa Krismasi inapaswa kuwa kipindi cha kutafakari, upendo na maridhiano miongoni mwa mataifa na jamii mbalimbali duniani.

    Wakristo kote ulimwenguni wanatarajiwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi kesho, wakikumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita.

    December 24, 2025

    Leave a Comment