BY ISAYA BURUGU 28TH JULY,2023-Rais mstaafu Uhuru Kenyatta hivi leo ameungana na  viongozi wa Azimio la Umoja kwa ibaada maalum kuwaombea familia za watu waliouawa kwenye mandamano yaliyondaliwa  maajuzi kupinga gharama ya juu ya Kimaisha.Hafla hiyo inaandaliwa katika mtaa wa mtaa wa karen.

Wengine wanaohudhuria hafla hiyo ni kinara wa Azimio Raila Odinga,kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka,aliyekuwa gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya,Mwangi wa Iria ambaye ni kiongozi wa chama cha Usawa ,katibu wa chama cha Julibilee Jeremiah Kioni miongoni mwa wengine.Kwenye hafla hiyo sala za kumuoma Mungu azipe nguvu familia zilizowapoteza wapendwa wao zimesheheni .

Hadi wakati wakuchapisha taarifa hii hafla hiyo ingali inaendelea.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

July 28, 2023