BY ISAYA BURUGU 11TH JAN,2022-Rais Wiliamu Ruto hivi leo ameongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu wa polisi wa utawala katika chou cha utoaji  mafunzo kwa maafisa hao iliyoko Embakasi Nairobi.Maafisa hao wanaofuzu wamekuwa katika mafunzo ya miezi tisa iliyopita.

Akihutubu katika hafla hiyo,rais hakukosa kurejelea hali tete ya kiusalama eneo la afrika mashariki na upembe mawa Afrika haswa na kusema kuwa serikali yake iko imara kuunga mkono juhudi za kukabili changamoto hiyo swa tatizo la wizi wa mifugo humu nchini.

Kwa kuzingatia adhari za mabadiliko ya hali ya hewa, rais Ruto ameviagiza vikosi mbali mbali vya kiusalama kushiriki kikamilifu katika upanzi wa miti.

.

Kwa upande wake Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amesema kuwa wizara yake imo mbiyoni kutekeleza wajibu wake katika kuhhakikisha kuwa wananchi wanaishi katika mazingira salama na yanayotii  haki za kila mmoja .

Hafla hiyo imehuhuriwa pia na naibu rais Rigathi Gachagua, gavana wa Nairobi Johnstone Sakaja ,inspekta mkuu wa polisi Japheth Koome kati ya maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini.

 

 

January 11, 2023