BY ISAYA BURUGU,30TH OCT,2023-Wakenya sasa wanaweza kununua simu za mkononi zilizotengenezwa nchini kwa gharama nafuu baada ya kuzinduliwa kwa kiwanda cha kutengeneza simu hizo  katika eneo la Athi River.Kiwanda hicho kimebuniwa kwa ushirikiano wa kampuni za utoaji huduma za simu humu nchini na mashirika yakimataifa yanayotengeneza simu.

Simu hizo zitakazopatikana katika maduka ya uzaji wa simu nchini na kwenye mitandao,zitauzwa kwa shilingi 7499.

Kiwanda hicho kwa jina East Africa device Asembly limited ambacho kinakuja kutimiza ahadi ya serikali ya kujenga kiwanda cha utengenezaji simu nchini,kimejengwa na uwezo wa kutengeneza simu milioni tatu kila mwaka.

Akizindua kiwanda hicho rais Wiliam Ruto amesema kiwanda hicho kitabuni mamia ya fursa za ajira.

 

 

 

Share the love
October 30, 2023