BY ISAYA BURUGU,6TH DEC 2023-Wizara ya Mambo ya Ndani inasema shule zilizofungwa kutokana na mashambulizi ya majambazi huko Pokot Magharibi zinatazamiwa kufunguliwa tena.

Akiwa katika ziara ya kukagua  shule zilizotelekezwa katika eneo hilo kufuatia visa vya ukosefu wa usalama,waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki anasema mchakato wa kurekebisha uaribifu uliotokea kwenye taasisi utafanywa kabla ya shule kufunguliwa Januari mwakani.

Kindiki alisema shule zitakazofunguliwa ni pamoja na Shule ya Msingi ya Chesegon, Shule ya Msingi ya Cheptulel, Shule ya Upili ya Wavulana ya Cheptulel, Shule ya Msingi ya Sapulmoi na Kisaa ECD katika Kaunti Ndogo ya Pokot ya Kati.Waziri huyo pia alidokeza kwamba mafunzo ya Askari Polisi wa Akiba 205 (NPR) yataanza Alhamisi katika Uwanja wa Chuo cha Ualimu cha Chesta katika Eneo Bunge la Sigor

.Watatumwa kusaidia Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) baada ya kumaliza mafunzo yao.Waziri pia ametangaza kuwa zoezi la upkonyaji silaha wakaazi wanaomiliki silaha eneo hilo kinyume cha sheria litaanzishwa hivi karibuni.

 

 

 

December 6, 2023