Maelfu ya wananchi katika maeneo mbalimbali wamejitokeza kutwa ya leo kushiriki katika maandamano yaliyoandaliwa na muungano wa Azimio la Umoja, kupinga serikali ya Rais William Ruto.

Jijiji Nairobi, waandamanaji walihusika katika makabiliano na maafisa wa polisi kwa kutumia mawe, huku polisi wakitumia vitoa machozi kuwakabili na kuwatawanya. Viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga, walijumuika na waandamanaji hao majira ya alasiri, na kuzunguka katika mitaa tofauti ya jiji hilo, huku maafisa wa polisi wakiwazuia kuingia katikati ya jiji.

Odinga na viongozi wenza wameendelea kushinikiza kushushwa kwa gharama ya Maisha, Pamoja na kufunguliwa kwa seva ili kuweka peupe matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Maandamano hayo yaliandaliwa licha ya Inspekta jenerali wa Polisi Japheth Koomekuwaonya watakaojihusisha katika maandamano yenyewe.

https://twitter.com/orengo_james/status/1640386461085184003?s=20

 

March 27, 2023