Hatimaye wabunge katika bunge la Kitaifa wameanza vikao vyao katika ukanda wa Pwani, baada ya kupata suluhu kwa mgogoro wa fedha za maendeleo ya maeneobunge almaarufu NG – CDF uliokuwa umesitisha vikao vyao.

Vuta nikuvute kuhusiana na kutolewa kwa fedha hizi ilisitisha vikao vya wabunge kwa muda wa siku mbili, wabunge wakisusia mkutano wao wakidai mgao wa fedha za NG – CDF unaotumiwa kutekeleza miradi katika maeneobunge tofauti kote nchini.

Spika wa bunge la Kitaifa Moses Wetangula, aliandaa kikao na wabunge hao na viongozi wa kamati mbalimbali ili kuafikia mwafaka huo, wakikubaliana kuongezewa shlingi bilioni 4 katika mpango huo.

January 25, 2023