25TH DEC,2023-Wakristo kote duniani wanasherehekia sikukuu ya Krismasi leo kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Kwenye mahubiri yake ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewakumbusha waumini juu ya umuhimu wa amani.

Anatarajiwa kurejelea mwito huo wakati wa ibada ya sikukuu hiyo atakayoiongoza leo mjini Vatican. Sikukuu ya mwaka huu inasherehekewa chini ya kiwingu cha vita vinavyoendelea huko Ukanda wa Gaza na nchini Ukraine.

Mjini Bethlehem inakoaminika Yesu Kristo alizaliwa, sherehe za kila mwaka za Krismasi zimefutwa ikiwa ni pamoja na shamra shamra na mapambo ya mji mzima ambayo huwavutia maelfu ya watalii.

Katikati mwa mji huo uliopo eneo la Ukingo wa Magharibi, bendera kubwa ya Palestina imetandazwa juu ya bango lenye ujumbe unaosomeka “kengele za Bethlehem zinagongwa kuhimiza usitishaji mapigano Ukanda wa Gaza.

 

 

 

December 25, 2023