BY ISAYA BURUGU,31ST OCT,2023-Wanasiasa watatu wa eneo la bbonde la ufa hivi leo wamehojiwa na kitengo cha upelelezi wa jinai huko Nakuru kufuatia mashambulizi na ghasia zilizoshuhudiwa hivi maajuzi katika kaunti za Baringo na SAMBURU.

Watatu hao mbunge wa Tiaty Wiliam Kamket ,mwenzake wa Sigor Peter Lochakapong na seneta wa Pokot Magharibi Julius Murgor wamehojiwa kuhusu mikutano ya kisiasa na matamshi waliyoyatoa kuhusu hali ya usalama katika kaunti ya Baringo na sehemu zingine ambazo serikali inaendesha oparesheni ya kurejesha usalama.

Watatu hao wanaripotiwa kukanusha madai yoyote ya kuchohea vita kuhusika kwenye uvamizi wa hivi maajuzi kwenye kambi ya maafisa wa GSU na shule ya msingi eneo la Kabindasum kaunti ya Baringo.

Wameachiliwa baada ya kuandikisha taarifa huku makachero wakiwamuru kujiwasilisha kila wakati wanapohitajika wakati uchunguzi ukiendelea.

 

 

October 31, 2023