Washukiwa wawili wa uvamizi katika dukakuu la Jamia katika kaunti ya Kisumu wakati wa maandamano ya kupinga serikali, waliokamatwa na kufikishwa mahakamani, wataendelea kuzuiliwa kwa siku 10 zaidi, ili kwapa muda maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi wao.

Taarifa kutoka kwa idara ya mashtaka ya Jinai DCI, ilieleza kwamba wawili hao Isaac Odhiambo and Peter Ochieng waliwasilishwa katika mahakama ya Kisumu, wakihusishwa na wizi wa bidhaa za kawaida katika duka hilo.

Taarifa hiyo ya DCI aidha imeweka wazi kwamba Washukiwa wengine 12 waliokamatwa kwa kushiriki katika shughuli za haribifu wakati wa maandamano hayo watawasilishwa mahakamani siku ya Jumanne wiki hii na kushtakiwa.

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1642179529518075905?s=20

April 1, 2023