BY  ISAYA BURUGU,23RD AUG 2023-Waziri wa michezo Ababu Namwamba  amekanusha madaui kuwa afisi yake imewapuuza wanariadha wa humu nchini,wanamichezo sawa na wanawake wanajihusisha katika michezo.

Akifika mbele ya bunge hivi leo Namwmaba ambaye alikuwa akijibu maswali kuhusu kuipuuza timu ya wanamichezo wenye mahitaji maalum waliokwenda kuwakilisha kenya katika mbio za dunia za olombiki kwa wanariadha wenye ulemavu  kule Berlin Ugerumani mnamo mwezi Juni mwaka huu,amesema wizara yake ilikaibidhiwa shilingi milioni 159 ili kuiwezesha timu hiyo kufanya mandalizi na kushiriki katika michezo hiyo.

 

Amesema kuwa maafisa 13 wa serikali  na wawili kutoka kwa wizara waliandamana na kiksoi hicho hadi nchini ujermani.Namwamba alikuwa akijibu maswali yaliyoibuliwa na kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichungwa aliyeataka kufahamu jukumu la wizara ya michezo katika kufanikisha mandalizi ya timu hiyo .Ababu alisema hakuwa nchini wakati timu hiyo ilipondoka kuelekea ugerumani lakini waliwezeshwa kikamilifu.

Share the love
August 23, 2023