BY ISAYA BURUGU,7TH NOV,2023-Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anasema mitihani inayoendelea ya KCSE itaendelea kama ilivyopangwa Jumatatu, licha ya siku hiyo kutangazwa kuwa sikukuu ya umma.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, Waziri wa Elimu alisema wanachama wote wa Kundi la Kusimamia Mitihani la Mashirika mengi wanapaswa kuripoti kazini kwa wakati ili kuhakikisha shughuli zote za siku hiyo zinatekelezwa vyema kama ilivyoratibiwa.

Katika notisi ya gazeti la serikali ya Novemba 6, Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki alisema Rais William Ruto ataongoza nchi katika zoezi la ukuzaji miti kulingana na mpango kabambe wa utawala wake wa kukuza miti bilioni 10 kufikia 2032.

Zoezi la upandaji miti pia litaangaziwa katika kaunti 47 zikisimamiwa na Mawaziri na Magavana, ambapo raia wote wa Kenya na umma kwa jumla watatarajiwa kushiriki.

Hatua ya kutangaza Novemba 13 kuwa sikukuu ya umma inafuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri lililoketi Mombasa mnamo Ijumaa, Novemba 3, 2023, kuhusu hitaji la kuokoa nchi kutokana na athari mbaya za Mabadiliko ya Tabianchi.

 

Share the love
November 7, 2023