John-Mbadi bajeti

    Waziri wa Hazina ya Kitaifa, John Mbadi, anatarajiwa kuwasilisha makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa kifedha katika kikao cha Bunge leo alasiri.

    Bajeti hiyo, ambayo imekadiriwa kuwa ya jumla ya shilingi trilioni 4.2, itabainisha maeneo muhimu ambayo serikali inapanga kutumia fedha zake, pamoja na mbinu mbalimbali zitakazotumika kukusanya mapato ya kuifadhili.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Hazina ya Kitaifa, serikali inalenga kukusanya takriban shilingi trilioni 2.7 kupitia ushuru, ada za huduma za serikali, pamoja na mikopo ya ndani na nje ya nchi.

    Hii itakuwa bajeti ya kwanza ya Waziri Mbadi tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, baada ya kuondolewa kwa Mswada wa Fedha wa mwaka 2024/2025 kufuatia maandamano makubwa yaliyoongozwa na vijana mwaka jana.

    June 12, 2025

    Leave a Comment