DCI

Waziri wa Usalama wa Ndani, Kithure Kindiki, ameweka wazi mipango ya kuboresha mfumo wa teknolojia katika Idara ya Upelelezi (DCI) nchini. Hatua hii inalenga kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa na DCI kwa umma.

Mipango hiyo imekuja baada ya mkutano kati ya Waziri Kindiki na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai Nchini, Mohammed Amin, uliofanyika asubuhi hii. Katibu wa Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa, Raymond Omollo, aliyeshiriki katika kikao hicho, ameeleza kuwa marekebisho ya mfumo wa teknolojia yatasaidia kuharakisha utoaji wa vyeti vya uadilifu na kupunguza mrundiko uliopo.

Malengo ya mipango ya kuboresha DCI ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya teknolojia, kutoa huduma za haraka, na kupunguza mrundiko wa maombi ya vyeti vya Uadilifu ambavyo vimekuwa vikiwatatiza wakenya wengi. Mipango ya kuimarisha huduma za DCI inajiri wakati ambapo waziri Kindiki anaendelea na mchakato wa kuimarisha huduma zinazotolewa na ofisi mbalimbali za umma.

 

September 12, 2023