Photo of SGR Train in Kenya

Waziri wa hazina ya kitaifa Ukur Yatani amejitokeza na kuweka wazi kuwa taifa la Kenya halijawahi kukataa au kuchelea katika ulipaji wa mkopo wowote uliokopwa kutoka kwa wakopeshaji wa nje na mataifa ya kigeni.

Yattani ametoa kauli hizi baada ya chapisho la gazeti moja la humu nchini kueleza kuwa serikali imeshindwa kulipa deni inayodaiwa na taifa la China la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Katika taarifa yake Alhamisi 13.10.2022, Yatani alifafanua kuwa benki za Uchina hazijatoza nchi faini ya Sh1.312 bilioni kwa kutolipa mkopo katika mwaka wa kifedha uliokamilika mwezi Juni.

Yattani ameitaja taarifa hiyo kama ya kupotosha huku akisisitiza kwamba viwango vya mikopo vya Kenya bado ni dhabiti na kuwa taifa halijawahi kuripotiwa kama nchi ambayo inaweza kukiuka majukumu yake ya kulipa deni.

Waziri  Yatani vilevile alisema kwamba,shughuli ya ulipaji wa madeni ya taifa hupewa kipaumbele katika bajeti ya matumizi ya serikali.

October 13, 2022