BY ISAYA BURUGU,07 NOV,2022- Mazungumzo  ya kusaka amani katika ya serikali ya Ethiopia na waasi katika taifa hilo  yameanza jijini Nairobi.

Mazungumzo hayo yanaongzwa na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta na rais wa zamani wa Nigeria Ole gusun Obasanjo.

Kundi la TPLF pia linahudhuria.Akizungumza katika mkutano huo Uhuru amelezea matumaini kuwa mazungumzo hayo yatafanikiwa na kurejesha utulivu na amani nchini Ethiopia.

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa kumekuwa na mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa TPLF eneo la Tigray nchni Ethiopia halia mbayo imepelekea maafa huku maelfu ya watu wakilazimika kuhama makwao.

 

November 7, 2022