Mgomo wa marubani umeingia siku ya tatu hii leo huku shuguli katika viwanja vya ndege zikiendelea kutatizika. Licha ya shirika la KQ kuongeza idadi ya safari, hali bado ni tete ikizingatiwa kwamba pande zote zimekosa kuafikiana.

Aidha afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Allan Kilavuka amesema kuwa nafasi ya kufanya mazungumzo ya makubaliano imefungwa na kuwaamuru marubani hao kurejea kazini au wapigwe kalamu. Kulingana na Kilavuka,marubani hao watawajibika kibinafsi kutokana na hasara ambayo imesababishwa na mgomo huo.

Vilevile ameongeza kuwa shirika hilo liko tayari kuwaajiri marubani wapya ili kuepuka kuwekwa mateka kila mara.Kando na hayo Kilavuka ameomba radhi kwa mgomo huo na kusema kuwa shirika hilo lilikuwa limerejelea asilimia 20% ya safari kufikia saa nane adhuhuri na kusafirisha takriban tani 25 za mizigo.

November 7, 2022