Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amewatolea wito wakristu kuliombea taifa la DR Congo, wakati hali ya machafuko ikiendelea kulikumba taifa hilo.

Katika waraka wa maombolezi kwa askofu wa kanisa la Church of Christ katika taifa hilo la Congo, Papa Francis ameeleza kusikitishwa na shambulizi lililotokea nchini humo siku ya Jumapili  katika kanisa moja na kuwaua washirika 14 huku wengine wapatao 40 wakiachwa kama wanauguza majeraha.

Wito sawa na huu umetolewa wa wakristu kuiombea roho ya marehemu Padre Isaac Achi wa Dayosisi ya Minna kaskazini mwa taifa la Nigeria, ambaye aliuawa siku ya Jumapili iliyopita katika makazi kwneye parokia. Watu wasiojulikana waliichoma nyumba ya padre katika kanisa hilo na kumwacha padre msaidizi Padre Collins Omeh na majeraha mabaya ya risasi alipokuwa akijaribu kujiokoa.

Taarifa ya papa inajiri huku wananchi wa DR Congo wakijiandaa kumlaki Papa Francisa mbaye atazuru taifa hilo mwaka ujao, pamoja na kufanya ziara katika taifa la Sudan Kusini.

January 18, 2023