Bunge la seneti linatarajiwa kuandaa kikao maalum hapo kesho ili kujadili mustakabali wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC miongoni mwa masuala mengine.

Ajenda ya kwanza ya maseneta watakaorejea kutoka likizo itakuwa ni kumapisha seneta mpya wa Elgeyo Marakwet William Kisang aliyetwaa wadhfa huo baada ya Kipchumba Murkomen kuwa waziri.

Kupitia notisi iliyochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali, spika wa bunge hilo Amason Kingi amesema kuwa kutaandaliwa vikao viwili, kikao cha kwanza kikianza mwendo wa 10.00 asubuhi hadi saa 12.30 adhuhuri huku kikao cha pili kikirejelewa kuanzia saa 2.30 adhuhuri.

January 18, 2023