Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi (EACC) imemkamata Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kaunti.

    Kulingana na wakili wa Natembeya Ndegwa Njiru, gavana huyo aliwasilishwa katika makao makuu ya EACC huko Nairobi leo asubuhi ili kurekodi taarifa kuhusiana na tuhuma hizo.

    Hata hivyo, ameeleza kuwa timu ya Natembeya ya wanasheria imekataliwa kumuona mteja wao na atasalia kizuizini hadi wakati usiojulikana.

    EACC imesema inachunguza madai ya makosa ya ununuzi, utumizi mbaya wa ofisi na hongo. Imeongeza kuwa kukamatwa kwa gavana huyo pia kunahusishwa na kupatikana kwa njia ya ulaghai wa KSH.1.4 bilioni.

    Tuhuma hizi zinaaminika kutokea katika miaka ya kifedha ya 2022/2023 hadi 2024/2025.

    May 19, 2025

    Leave a Comment