Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) inashirikiana na mamlaka husika kumwajibisha aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua kwa matamshi yake yaliyoonyesha uwezekano wa ghasia katika uchaguzi wa 2027, ambazo alilinganisha na zile za mwaka wa 2007.

    Mwenyekiti wa NCIC, Samuel Kobia, Jumatano alisema hakuna sherehe kuhusu kipindi hicho ambacho kilikumbwa na vifo, uharibifu na kufurushwa kwa watu.

    Kobia alisema kwamba Gachgua hakujali kumbukumbu za waathiriwa na ujasiri wa walionusurika.Tume hiyo pia ilitoa onyo kwa viongozi wengine, ikiwataka kuzingatia matamshi yao katika mikutano ya hadhara au mahojiano kwenye vyombo vya habari.

    May 21, 2025

    Leave a Comment