Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu amesema kuwa tatizo la ukosefu wa taa za barabarabi mjini Narok litatuliwa hivi karibuni.

    Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Ntutu amekiri kwamba ukosefu wa taa hizo umechangia ukosefu wa usalama mjini humu, akisema kuwa kampuni ya Kenya power itashugulikia suala hilo ili kuwezesha wafanyabiashara kuendeleza biashara zao bila tashwishi nyakati za usiku.

    Aidha ameshikilia dhamira ya serikali yake kubuni mazingira mazuri ya biashara. Kwa muda sasa wakaazi wa Narok mjini wamekuwa wakihangahika nyakati za usiku kufuatia ukosefu wa taa za barabarani.

    July 22, 2025

    Leave a Comment