Mahakama Kuu imeipa serikali pigo kubwa baada ya kusitisha matumizi ya lazima ya Mfumo wa Ununuzi wa Kielektroniki(e-procurement). Katika uamuzi wa Jumatatu, mahakama ilisema mashirika ya umma yako huru kupokea na kuwasilisha hati za zabuni kwa njia ya kielektroniki au la mradi tu yanakidhi matakwa ya Sheria ya Ununuzi na Utoaji wa zabuni.

    Hazina ya kitaifa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ziliamriwa zaidi kushughulikia mawasilisho ya kielektroniki na ya mikono kwa usawa.

    Mfumo wa e-procurement ulikuwa sehemu ya mageuzi yaliyoungwa mkono na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kurahisisha manunuzi ya serikali na awali uliwekwa kuanza kutumika mwaka wa 2024.

    Aidha waziri wa hazina ya kitaifa kupitia mtandao wake wa X alisema kuwa serikali haitalegeza kamba katika kutekeleza mfumo huo.

    September 9, 2025

    Leave a Comment