Karibia miezi miwili baada ya gavana wa Narok Patrick Ntutu kuahidi kuwa kampuni ya umeme ya Kenya power tawi la Narok, itatatua tatizo la ukosefu wa taa za barabarani, baadhi ya wakaazi wa Narok mjini wameibua malalamishi wakisema kuwa taa hizo bado hazijaweza kushugulikiwa.

    Kulingana na wakaazi hao ambao wamezungumza na kituo hiki cha Radio Osotua, ukosefu wa taa hizo umeathiri pakubwa biashara zao hasa majira ya usiku ikizingatiwa kuwa wanalazimika kufunga biashara zao mapema, wakihofia usalama wao kutokana na giza.

    September 17, 2025

    Leave a Comment