Askofu mstaafu wa jimbo katoliki la Kakamega Philip Sulumeti ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88. Taarifa ya kifo cha askofu Sulemeti, ilitangazwa na askofu wa sasa wa jimbo la Kakamega Joseph Obanyi.

    Askofu Obanyi, alituma salamu za rambirambi kwa familia ya Sulumeti, marafiki na watu wa Jimbo hilo. Mhashamu Sulumeti aliyezaliwa mnamo Agosti 15, 1937, katika kijiji cha Kotur, Teso Kusini, Kaunti ya Busia, alitawazwa kuwa padre mjini Kisumu mnamo Januari 6, 1966.

    Aliteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Kisumu mwaka wa 1972 na akawa Askofu Mkuu wa Urci akiwa na umri wa miaka 35, cheo kinachohusishwa na jimbo ambalo halifanyi kazi tena.

    Alitawazwa kuwa askofu mnamo Agosti 20, 1972, akateuliwa kuwa Askofu wa Kisumu mnamo Desemba 9, 1976, na kuwa Askofu wa Kakamega mnamo Februari 28, 1978.Alistaafu Desemba 5, mnamo 2014.

    November 10, 2025

    Leave a Comment