Tovuti za serikali ambazo zilikuwa zimedukuliwa zimerejeshwa. Katika taarifa katibu katika wizara ya Usalama wa Ndani Raymond Omollo alithibitisha kisa hicho, akisema hali hiyo imedhibitiwa kikamilifu.
Omollo alisema ukiukaji huo ulifanya tovuti kadhaa za serikali kutoweza kufikiwa kwa muda, akiongeza kuwa matokeo ya awali yanaonyesha shambulio hilo lilitekelezwa na kundi linalojiita “PCP@Kenya.
Kulingana naye, timu za kiufundi zilifanya kazi na washikadau ili kuleta utulivu na kurejesha majukwaa yaliyoathiriwa.
Alishikilia kuwa juhudi zinaendelea ili kuimarisha ulinzi na kuzuia matukio kama hayo kwa kuhakikisha kwamba vitisho vya mtandao vinagunduliwa mapema.
Baadhi ya tovuti zilizoathirika ni pamoja na tovuti za wizara ya elimu, wizara ya afya, wizara ya usalama wa ndani miongoni mwa zingine.
In an era defined by a disruptive digital shift, Kenya faces rising cyber threats ranging from online scams, SIM-swap fraud to attacks on critical systems and acts of digital cruelty that undermine dignity.
Even as we modernize public services under the Bottom-Up Economic… pic.twitter.com/JV9gT5OWrc
— Dr. Raymond Omollo — CBS (@ray_omollo) November 17, 2025

