Rais William Ruto ameagiza wanafunzi wote kuripoti shuleni kuanzia Ijumaa, licha ya vikwazo vyao vya kifedha au ukosefu wa sare.

    Akizungumza huko Meru wakati wa utoaji wa fedha chini ya mpango wa NYOTA, Rais Ruto amewaagiza machifu kutekeleza agizo hilo ili kuhakikisha watoto wote wanaripoti shuleni kwa masomo yao ya muhula wa kwanza.

    Kiongozi wa Nchi alidai kwamba serikali ilitoa Ksh.44 bilioni kwa ajili ya elimu na hakuna mtoto anayepaswa kunyimwa fursa ya kupata elimu kutokana na ukosefu wa karo za shule.

    Alisema kwamba mpito kutoka shule ya msingi hadi shule ya upili, chini ya Mtaala mpya wa CBE, hayapaswi kulemazwa kutokana na vikwazo vya kifedha na utawala.

    January 22, 2026

    Leave a Comment