Kamati ya fidia ya waathiriwa wa maandamano imeonya wanasiasa dhidi ya kuiingiza siasa katika mchakato wa fidia.Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) na Kamati inayosimamia Utekelezaji wa Ajenda ya Pointi Kumi na Ripoti ya NADCO (COIN-10) imewashauri wanasiasa kutoingilia suala hilo.

    Mwenyekiti wa KNCHR Claris Oganga na makamu mwenyekiti wa COIN-10 Javas Bigambo walisema wanaunda mfumo wa kutekeleza mchakato wa fidia kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kuunda orodha iliyothibitishwa ya waathiriwa wa maandamano wanaotarajiwa kulipwa ifikapo Juni mwaka huu.

    Walipokuwa wakihutubia waandishi wa habari Jumatatu, timu hiyo iliwasihi waathiriwa wa ukatili wa polisi kuendelea kuripoti kesi hizo kabla ya dirisha la siku 21 kufungwa.

    March 16, 2026

    Leave a Comment