Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua hii leo amezuru mji wa Narok ambapo amewahutubia wananchi katika eneo la rungu ya Moi.

    Gachagua aliandamana na viongozi mbalimbali akiwemo kinara wa wiper Kalonzo Musyoka, Kinara wa PLP Martha Karua, Eugene wamalwa wa DAP-K pamoja na aliyekuwa mwanasheria mkuu Justin Muturi.

    Kiongozi huyo wa DCP, ameendeleza kampeni zake dhidi ya utawala wa Kenya Kwanza akidai kuwa mkuu wa nchi rais William Ruto amenyakua mashamba mengi katika kaunti ya Narok.

    Kwa upande wa viongozi walioandamana na Gachagua, wamekashifu vikali visa vya vijana kukamatwa kiholela na wengine hata kutoweka.

    June 30, 2025

    Leave a Comment