BY ISAYA BURUGU ,15TH NOV,2022- WITO umetolewa kwa  wafanyibiahsara sawa na taasisi za kifedha katika kuaunti hii kujitolea katika kuwasaidia walioadhirika na baa la njaa kufuatia uukame unaendelea kushudiwa katika sehemu mbali mbali za nchi sawa na kaunti hii ya Narok.

Ni wito wake Askofu wa  kanisa la PAG Narok John Ole Mpurkoi Akizungumza na wandishi Habari mjini Narok askofu Mpurkoi amesisitiza haja ya wahisani wote walio na uwezo kujitokeza na kuwasaidia wengi ambao anasema wanaendelea kutaabika kutokana na baa hilo la njaa.Antony Mintila ana kina cha taarifa hiyo

.Ametangaza kuwa viongozi wakidini katkika kaunti ya Narok wako tayari kupokea chakula hicho na misaada mingine yoyote kutoka kwa wahisani na kukipeleka katika afisi ya kaunti kamishna wa Narok  ili kukisambaza kwa walengwa.

Pia ameitaka serikali kuu kuendelea na juhudi zake za kusambaza chakula kwa walioadhirika hadi hali itakaporejelea kuwa shwari.

 

November 15, 2022