BY ISAYA BURUGU 1TH NOV,2022-Tajiri  wa Marekani Bill Gates yuko humu nchini ambapo amepangiwa  kufanya msururu wa mazungumzo ya umma.Mwanzilishi huyo wa Microsoft anatazamiwa kukutana na maafisa wa serikali na washikadau wengine katika sekta ya kibinafsi.Gates atazuru kaunti ya Makueni ambako atakaribishwa na Gavana Mutula Kilonzo Jnr.Ripoti zinadokeza kuwa atatembelea hospitali ya Makueni Mother and Child hospital na Kituo cha Afya cha Kathonzweni.

Pia atatembelea viongozi mbalimbali, washirika, na wafadhili na pia kukutana na wanasayansi wa kikanda na wavumbuzi.Gates atatangaza kujitolea kwa Bill & Melinda Gates Foundation kuunga mkono ubunifu mpya unaolenga kuboresha afya, usalama wa chakula, na usawa wa kijinsia katika nchi za Afrika.

Pamoja na viongozi wa Bill & Melinda Gates Foundation, watatembelea na kujifunza kutoka kwa wakulima wanaotumia zana za kidijitali kusaidia kukabiliana na hali ya hewa, kuona jinsi kliniki za afya ya msingi zilivyotoa huduma wakati wa janga na kusaidia kukabiliana na matishio yanayoendelea kama vile VVU, TB na malaria.

Mwanzilishi wa Bill and Melinda Foundation alitembelea kenya mara ya mwisho mwaka wa 2016 na kukadiria ubunifu wa vijana wa Kenya.

 

November 15, 2022