Radio Osotua › Local News

Askofu wa CITAM David Oginde ateuliwa kuiongoza EACC.

Local News March 11, 2023 John Waicua

Rais William Ruto amemteua Askofu (Dkt.) David Adang Oginde kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC.)

Uamuzi wa kumteua Askofu Oginde unafuatia pendekezo la Tume ya Utumishi wa Umma (PSC). Oginde atachukua nafasi ya Askofu Mkuu (Mstaafu) Dkt. Eliud Wabukala ambaye amestaafu baada ya kuwa mwenyekiti wa tume ya EACC kwa kipindi cha miaka sita.

Hata hivyo, uteuzi wa mwenyekiti mpya unahitaji kuidhinishwa na wabunge kabla yake kutwaa hatamu katika ofisi hiyo. Aliyekuwa Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana na Amani Komara pia walikuwa wamependekezwa na PSC.