Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga amezuru hii leo ametua eneo la Ewasonyiro Narok kusini kuendelea kuzungumza na wananchi kuhusu kile wanachotaja kuwa ni serikali ya rais Wiliam Ruto kushindwa kukabili changamoto zinazowakumba wananchi.

Akiwahutubia wakaazi wa Ewasonyiro Odinga amesema serikali ya Kenya Kwanza imezamisha ndoto ya wengi katika taifa hili kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha na kuweka wazi kuwa anapanga maandamano katika jiji kuu la Nairobi tarehe 20 mwezi huu katika hatua ya kushinikiza serikali kuteremsha bei ya bidhaa muhimu za matumizi. 

Kauli ya Odinga imeungwa mkono na Martha Karua na Kalonzo Musyoka ambao wamesema serikali ya Kenya kwanza imekandamiza mwananchi wa kawaida na wakati umewadia wakenya kuungana kupigania haki yao.

Naye kwa upande wake seneta wa kaunti hii ya Narok Ledama Ole Lekina  amesema serikali lazima iwape haki wakazi kaunti ya Narok.

Akizungumza katika eneo la Ewaso ng’ro wakati wa mkutano wa azimio la umoja, Ledama amemtaka Rais William Ruto kulinda msitu wa mau kama alivyoahidi wakati wa kampeni zake kauli ambayo imeungwa mkono na aliyekuwa mbunge wa Narok kaskazini Moitalel Ole Kenta.

March 11, 2023