Askofu John Lelei amesimikwa rasmi kama askofu wa kwanza wa jimbo jipya la Kapsabet ambalo lilianzishwa na papa Leo wa XIV July 10 mwaka huu.
Hadi uteuzi wake, mhashamu Lelei, alikuwa askofu msaidizi katika jimbo la Eldoret na aliteuliwa kuongoza jimbo hilo jipya, ambalo lilibuniwa kutoka kwa jimbo katoliki la Eldoret.
Ibada ya misa takatifu imeandaliwa katika kituo cha michezo cha Eliud Kipchoge na kuongozwa na mwakilishi wa Papa nchini Kenya askofu mkuu Bert Van Megen. Katika homilia yake, askofu mkuu Megen amemhimiza askofu Lelei kufuata mfano wa Yesu wa kuwatumikia wakristu.