Olposimoru

Maafisa wa polisi katika kituo cha Olposimoru, Narok Kaskazini, wamemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumwua mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 12 katika kijiji cha Kipendeni eneo la Olengape.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa Idara ya Upelelezi (DCI), mwanaume huyo amefahamika kwa jina la Samuel Landichi mwenye umri wa miaka 62. Inaelezwa kuwa mshukiwa alimkata mwanawe kwa panga kichwani, tukio ambalo lilisababisha kifo cha papo hapo. Sababu ya tukio hili la kushangaza bado hazijabainika, huku uchunguzi zaidi ukianzishwa ili kutambua kilichosababisha mwanaume huyo kuchukua hatua hii ya kikatili.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Olenguruoni huku upasuaji wa maiti ukitarajiwa kufanywa huku naye  mshukiwa akiendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Olokurto.

 

Share the love
September 21, 2023