Mahakama ya Mizozo ya Vyama vya Kisiasa imeongeza muda wa agizo la kukizuia chama cha ODM kuwatimua Seneta wa Kisumu Tom Ojienda na wabunge Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o na Elisha Odhiambo kutoka kwa chama hicho.

Mahakama hiyo pia iliagiza kesi hiyo itajwe tarehe 3 Oktoba kwa maelekezo zaidi.Chama hicho vilevile kimeagizwa kuwasilisha majibu yao kwa maombi ndani ya siku 5.

Ojienda, Odhiambo na Jalang’o walifurushwa pamoja na wabunge Caroli Omondi (Suba Kusini) na Gideon Ochanda (Bondo) lakini wakaelekea kortini na kupata maagizo ya kuzuia kufurushwa kwao.

Share the love
September 22, 2023