Bajeti ya taifa ya mwaka ujao wa kifedha inatarajiwa kuongezeka kwa shiling bilioni 251, na kufikia shilingi trilioni 3.6, kwa mujibu wa Nakala rasimu ya bajeti hiyo iliyotolewa, kabla ya kusomwa kwa bajeti ya taifa mwanzoni mwa kipindi kijacho cha fedha kuanzia mwezi Julai.

Waziri wa hazina ya kitaifa na Mipango ya Kiuchumi nchini Prof. Njuguna Ndung’u, bajeti hiyo itajumuisha mipango ya kubadilisha mkondo wa maisha ya wakenya pamoja na mapangilio ya kufanikisha maendeleo katika siku za usoni.

Baadhi ya mambo mengine yaliyo katika nakala rasimu ya nbajeti hiyo ni pamoja na kilimo, biashara ndogo, ndogo na za kati, makaazi, Huduma ya afya; ukuaji wa kidijitali na tasnia ya ubunifu.

February 16, 2023