Wananchi katika kaunti ya Narok wataendelea kushuhudia vipindi vya ukame katika kipindi kilichosalia cha mwezi huu wa Februari, kabla ya kuanza kwa mvua fupi mwezi ujao.

Mkurugenzi mkuu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa katika kaunti ya Narok Bw. Peter Runanu, alieleza kwamba huenda hali ya mawingu ikatawala baadhi ya maeneo ya kaunti hii, ila uwezekano wa mvua kunyesha katika maeneo hayo ni finyu sana.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee kwa njia ya siku wakati wa kipindi cha Dira ya kazi mapema leo, Bw. Runanu amesema wananchi wengi huenda wakachukuia uwepo wa mawingu kama ishara ya mvua, ila ameeleza kwamba utabiri wao umeashiria kwamba uwepo wa mawingu utatawala sana, huku maeneo machache yakishuhudia rasharasha za mvua.

SAUTI | Bw. Peter Runanu – Mkurugenzi wa Idara ya Utabiri wa Anga, Narok.

February 16, 2023