Kawira Mwangaza

Magavana kupitia baraza la magavana nchini, wamejitokeza na kusimama namwenzao Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, wakati mswada wa kubanduliwa mamlakani ukitarajia kusikilizwa kwenye bunge la seneti hio kesho Jumanne 20.12.2022.

Katika taarifa yao kwa wanahabari adhuhuri ya leo katika jingo la Delta jijini Nairobi, Magavana wamewaomba maseneta kujikita katika sheria kabla ya kufanya maamuzi ya kumwondoa mamlakani gavana mwangaza, wakati wataanza kusikiliza vikao hivyo.

Gavana kawira mwangaza alibanduliwa mamlakani na wawakilishi wadi katika kaunti ya Meru juma lililopita, na sasa anasubiri kujua hatma yake iwapo ataendelea na wajibu wake au atang’atuka.

Wakati hayo yakijiri, spika wa Bunge la seneti Amason Jeffa Kingi ameitisha kikao maalum cha bunge hilo hiyo kesho Jumanne kutathmini hoja ya kumwondoa mamlakani gavana Mwangaza iliyopitishwa na bunge la kaunti ya meru tarehe 14 mwezi huu.

Kingi kupitia notisi rasmi kwenye gazeti la serikali iliyochapishwa tarehe 16 mwezi huu ametangaza kuwa kikoa hicho kinafuatia ombi kutoka kwa  kiongozi wa wengi Aaron Cheruiyot  na spika wa bunge la Meru Ayub Bundi  kujadili swala hilo. Kingi ameongeza kuwa  kikao hicho kitaandaliwa  katika majengo ya bunge la seneti  kuanzia  saa nane unusu kesho Jumanne.

Mwangaza aling’atuliwa baada ya wawakilishi wadi 67 wa bunge la Meru kupigia kura hoja ya kung’atuliwa kwake. Hoja hiyo ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na mwakilishi wadi wa Abogeta magharibi Dennis Kiogora tarehe 22 mwezi Novemba. Wawakilishi wadi hao wanamtuhumu gavana Mwangaza kwa kukiuka katiba na matumizi mabaya ya mamlaka.

December 19, 2022