Spika wa seneti Amason Jeffa Kingi  ameitisha kikao maalum cha bunge hilo hiyo kesho jumanne kutathimini hoja ya kumwondoa mamlakani gavana wa Meru  Kawira Mwangaza iliyopitishwa  na bunge la kaunti ya meru tarehe 14 mwezi huu wa Disemba.

Kingi kupitia notisi rasmi kwenye gazeti la serikali iliyochapishwa tarehe 16 mwezi huu ametangaza kuwa kikoa hicho kinafuatia ombi kutoka kwa  kiongozi wa wengi Aaron Cheruiyot  na spika wa bunge la  Meru Ayub Bundi  kujadili swala hilo.

Kingi ameongeza kuwa  kikao hicho kitaandaliwa  katika majengo ya bunge la seneti  kuanzia  saa nane unusu kesho jumane.

Mwangaza aling’atuliwa baada ya wawakilishi wadi 67  wa bunge la Meru kupigia kura  hoja ya kung’atuliwa kwake.

Hoja hiyo ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na mwakilishi wadi wa Abogeta magharibi Dennis Kiogora  tarehe 22 mwezi Novemba.

Wawakilishi wadi hao wanamtuhumu gavana Mwangaza kwa kukiuka katiba na matumizi mabaya ya mamlaka.

December 19, 2022