BY: BRIGIT AGWENGE/5TH OCT 2022-Muuguzi wa Kenya aliyekufa maji wakati akiogelea kwenye bwawa nchini Canada anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Motonto, kaunti ya Kisii.Hellen Wendy Nyabuto alikuwa akishirikisha marafiki wake katika kipindi cha moja kwa moja kwenye Facebook mnamo Agosti 18 wakati alipokumbana na kifo chake baada ya kuwezwa na nguvu za maji na kwa bahati mbaya kuzama.Mwili wake ulikuwa umehifadhiwa katika mochari ya Canada hadi wiki jana wakati familia yake ilipoenda kuuchukua kwa ajili ya mazishi. Baada ya kufanikiwa kuuchukua mwili, wazazi wa marehemu waliusafirisha kwa ndege ya shirika la ndege la  Ethiopian Airliness na kuwasili JKIA  Jumamosi iliyopita.Mwili wa Wendy ulilazwa katika chumba cha Lee hadi hiyo jana ambapo  ulipochukuliwa  kusafirishwa hadi nyumbani kwao Kisii.Hafla ya mazishi ya Wendy inafanyika, takriban mwezi moja unusu baada yake kuaga dunia huko Canada.

 

 

 

 

 

 

October 5, 2022