BY ISAYA BURUGU,3RD NOV,2023-Wanafunzi watano waliozama na kufa maji walipokuwa wakijiburudisha katika buastani ya Amazement park mjini Eldoret wanazikw ahivi leo.Milli hiyo imeondolewa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa na mafunzo mjini Eldoret.

Itakumbukwa kuwa wanafunzi hao walikuwa wafanye mtihani wa KCPE.Ibaada ya mazishi imeandaliwa katika shule ya msingi ya Arap Moi shule ambayo wanafunzi hao walikuwa wakisomea.Mbunge wa eneo bunge la Anapkoi Samuel Chepkonga amelezea kusikitishwa kwake na vifo vya kushangaza vya wanafuzni hao AKIWATAJA KAMA Watoto waliokuwa werevu.

Watoto hao walizama baada ya kudaiwa kupanda juu ya mashua yenye uwezo wa kubeba watu watatu huku vijana sita wakipanda juu ya chombo hicho hatua inayosemekana kuchangia kuzama kwake.Aidha mbunge huyo amekuwa na ushauri kwa walimu.

 

 

Share the love
November 3, 2023